Wauguzi
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara pamoja na uongozi wa
hospitali hiyo wameitaka idara ya boharia ya dawa nchini (MSD) kuondoa
urasimu wa ucheleweshwaji wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuepuka
wagonjwa kubaki wodini kwa muda mrefu wakisubiri matibabu na pia urasimu
huo husababisha vifo vinavyochangiwa na ukosefu wa dawa kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani
katika sherehe zilizofanyika kwa maandamano ya wauguzi wa hospitali hiyo
kama kumbukumbu ya muasisi wa shughuli za uuguzi duniani Bi Florence
Nightngale aliyezaliwa mei 12 1820 nchini Italia, huku mganga mfawidhi
wa hospitali hiyo Dr Manyama Deogratius akitolea ufafanuzi wa changamoto
za hospitali hiyo kukabiliwa na dawa na vifaa tiba kuwa husababishwa na
mlolongo mrefu katika idara ya boharia unaochukua siku 14 hadi mwezi na
kuitaka MSD kukiri ikiwa hawana dawa na ngazi ya mkoa itoe kipaumbele
kwa upatikanaji wadawa kwa haraka.
Awali katika risala ya wauguzi wa hospitali hiyo kwa afisa masuhuri
(katibu tawala mkoa) wamemueleza bayana kuwa licha ya hospitali hiyo
kuanza kutoa huduma yake 2013 inakabiliwa na upungufu wa majengo na
kutokamilika, pamoja na kuwepo kwa wauguzi 68,lakini ongezeko hilo
halikidhi mahitaji kutokana na kuongezeka kwa huduma na kasi ya wagonjwa
wasiopata huduma ya tiba.
Kwa upande wake kaimu afisa masuhuri (katibu tawala mkoa Manyara Bw
Masaile Mussa licha ya kusisitiza nidhamu kwa wagonjwa na kukemea
vitendo vya rushwa na ukatili kwa wauguzi bila ya kukiuka kiapo, lakini
akisisitiza serikali kutambua changamoto zilizopo zikiwemo za zikiwepo
za kuongeza wauguzi na kupandisha madaraja.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya wauguzi mwaka huu yaa kumuenzi
Muasisi Bi Florence Nightngale-wauguzi nguvu ya mabadiliko, huduma
fanisi na gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment