Wakuu
wa nchi za jumuiya ya afrika mashirika wamelaani jaribio la mapinduzi
yaliyotaka kufanyika nchini burundi huku wakitaka utawala wa sheria
kwa kuheshimu katiba na makubaliano ya arusha pamoja na kusogezwa mbele.
Akisoma maazimio ya mkutano huo mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais
Jakaya Kikwete amesema wanatambua hali ya kisasa iliyotokea burundi na
hivyo wanasisitiza makubaliano ya Arusha yaheshimiwe.
Mkutano huo umekubaliana kwa pamoja uchaguzi wa burundi usogezwe mbele hadi hali ya siasa itakapotengemaa.
Tofauti na matarajio ya wengi Rais Pierre Nkurunziza hakuweza
kuhudhuria mkutano huo licha yakuwepo taarifa kuwa aliwasili jijini Dar
es Salaam.
Hata hivyo mkutano huo hakuweza kufanyika katika utaratibu ambao
umepangwa kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kuwepo mapinduzi nchini Burundi
ambapo taarifa hizo zimeibua taharuki na wasiwasi miongoni mwa
washiriki wa mkutano huo wakiwemo viongozi kutoka nchi wanachama
No comments:
Post a Comment