Na Richard Bakana-shaffihdauda.com.
Wachezaji
wa klabu ya Liverpool jana katika mchezo wa ligi kuu ya England (EPL)
walipokutana na mabingwa wapya wa ligi hiyo Chelsea waliwaonyesha
heshima yao ya kubeba ubingwa, kitendo ambacho hata hapa Nyumbani
Tanzania kwa mara ya kwanza kilionyesha na klabu ya Azam FC ambao
waliwapigia makofi Yanga siku ya Jumatano timu hizo zilipokutana katika
Uwanja wa Taifa.
Mchezo
huo ambao ulipigwa Nyumbani kwa Chelsea ‘Stamford Bridge’ ulimalizika
kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kufungana bao moja moja.(P.T)
Chelsea
ndio walianza kupata bao kupitia kwa nahodha wake John Terry kunako
dakika ya tano (5) lakini mkongwe wa Liverpool ambaye anataka kuikimbia
timu hiyo Steven Gerrard akasawazisha bao hilo katika dakika ya 44
kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kugawana pointi moja moja na
goli 1-1.
Gerrard
alitumia mchezo huo kuwaaga mashabiki wake ambapo alipotoka Uwanjani
dakika za mwisho mwisho za mchezo huo, alienda katika upande wa
mashabiki wa Chelsea na kuwapungia mkono na wao wakaonyesha heshima kwa
kusimama na kumpigia makofi hari kadharika kwa mashabiki wa Liverpool.
Nguli
huyo ambaye maisha yake ya soka yalianzia hapo hapo Liverpool akiwa na
miaka nane sasa baada ya msimu huu kumalizika anatarajia kutimkia nchini
marekani kumalizia soka lake la uzeeni.
No comments:
Post a Comment