Mkuu wa wilaya ya misenyi FADHILI NKURLU ametoa onyo la mwisho kwa walimu wanao jaribu kuwafukuza wanafunzi nwenye ulemavu wa ngozi albino kwa kudai michango ya shule bila utaratibu maalumu.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya misenyi FADHILI NKURLU katika hafla ya kupata chakula cha mchana na watu wenye ulemavu wa ngozi albino wilayani misenyi ambapo amesema mwalimu atakae thubutu kumfukuza mtoto mwenye ulemavu waongozi albino au mtoto wa mtu mwenye ulemavu kwa kumdai gharama yoyote shuleni atachukuliwa hatuka akali za kisheria.
Mapema akiongea katika hafla hiyo mwenyekiti wa chama cha albino mkoa wa kagera BUCHARD EMMANUELI ameeleza changamoto na misukosuko ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo kwa kuhofia kuwawa huku akiomba serika kuwapatia gharama za usafili ili waweze kufika katika mkutano mkuu wa kimataifa wa siku ya albino duniani utakao fanyika jijini Arusha kwaanzia tarehe tisa mwezi wa sita na kuhakikisha ulinzi unaimarisha ili waweze kuishi kwa amani kama watu wengine.
Katika hafla hiyo watu wote wenye ulemavu wa ngozi albino wa wilaya ya misenyi walipatiwa bima za afya kwaajili ya kupata matiba bure bila gharama yoyote pamoja na simu za mkononi kwaajili ya kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pindi watakapo kuwa wana watilia mashaka watu wasiowema wanaotaka kuhatarisha maisha yao.
No comments:
Post a Comment