Nyumba kadhaa zimeboka na nyingine 80 kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa mawili katika vijiji vya kitete na kadudu wilaya ya kilosa mkoani morogoro na kusababisha uharibifu wa mazao na baadhi ya familia kukosa makazi.
Wakizungumza kwa huzuni wananachi wa vijiji vya kitete na kadudu wameeleza mvua zimesababisha madhara makubwa ikiwemo nyumba kuanguka na kusababisha baadhi ya kaya kukosa makazi ambapo kwa sasa wananchi hawana chakula kutokana na vyakula kuharibika baada ya kujaa maji huku mazao yaliopandwa mashambani yakiwemo mahindi yameseombwa na mvua na kuomba serikali kuwasaidia chakula wanachi waliokubwa na mafuriko.
Akitoa tarifa za tathmini ya awali ya mafuriko hayo afisa tarafa wa tarafa ya dumila MOSES NCHIMBI amesema nyumba zilizo anguka kabisa ni nane na nyingine 80 zimeharibika vibaya na kujaa maji ambapo ameeleza chanzo cha athari hizo hayo ni kuziba kwa mto DYONGOYA kutokana na baadhi ya wananchi kulima kando ya mto huo.
Mkuu wa wilaya ya kilosa BWANA JOHN NJEWELE amewapa pole wananchi wa vijiji hivyo kwa athari walizozipata ambapo ameagiza watendaji wa vijiji kata na vitongoji kuanza zoezi la kukagua na kubaini wananchi waliolima na kujenga kando kando ya mito na kusabaisha mito kuziba na maji kupoteza uelekeo na kujaa katika makazi ya wananchi.
No comments:
Post a Comment