Sunday 3 May 2015

Ajali ya boti yaua mmoja na kujeruhi wengine kadhaa baada ya kuzama baharini baada ya kupinduka.


Mtu moja amepatikana akiwa amekwisha fariki dunia kati ya watu watatu walio zama baharini baada ya kupinduka na FAIBA BOT huko wesha katika wilaya chake chake huku ikiwa watu wawili bado kupatikana hadi zoezi la uokozi lilipo fungwa rasmi hivi leo.

Wakitangaza kufunga kwa zoezi hilo uongozi wa mkoa kusini pemba kamanda wa polisi mkoa kusini pemba Juma Yusufu ali na mkuu wa mkoa huo Bimwana Juma Majid Abdalla walio kuweko eneo la tukio likoni wesha wamesema kazi ya uokozi ilikwenda kwa kasi na kufanikiwa kupata mtu moja akiwa amekwisha fariki huko bandarini mkumbuu .
Wamemtaja alie patikana kuwa ni Ali Mbarouk Salehe 55 mkazi wa mitamani chake chake na waleambao bado hawaja onekana kuwa ni Rashid Zahor na Omar Najimu Kibete wwote wakaazi wa mkoroshoni.
Akizungungumzia tukio hilo moja wa manusura wa ajalio  hio alie kuwemo ndani ya boti hio Ahmed Nasor 52 amesema jitihada za kutaka kuwaokoa wenzao hao ilifanyika ilakwavile hakukua na chombo karibu  ndio ilio pelekea wenzao hao kupotea nae moja wa waokozi  amesema wamefanikiwa kupata vifa walivyo kuwa navyo watuhao baada ya kuzamia katika boti yao ambayo ipo chini ya bahari nawalipo ikagua hakuna mtu hata moja.
Jitihada kubwa za kuwatafuta ilifanyika katika mwambao wa bahari ya eneo la pemba chanal walipo zama watu hao kwa kutumia boti ngalawa watembea kwa miguu kwenye mikoko na ndenge aina ya chata ambayo imezunguhadi mwambao wa tanga.

No comments: