Rais
Filipe Nyusi wa Msumbiji (kushoto) akiwapungia wananchi waliojitokeza
kumpokea wakati akiwasili Ikulu, Dar es Salaam jana kwa ziara rasmi ya
siku tatu. (Picha na Yusuf Badi)
RAIA wa
Tanzania na Msumbiji watakaotaka kuingia katika nchi hizo na kukaa wa
miezi isiyozidi mitatu, hawatalipia viza kama ilivyokuwa awali,
imeelezwa.
Aidha,
imetangazwa pia kuwa, wanafunzi kutoka katika nchi hizo kuanzia sasa
wanaruhusiwa kusoma kokote ndani ya Msumbiji na Tanzania wakitumia
pasipoti zao zitakazogongwa viza bure, kwa kipindi chote cha masomo yao,
hata kama ni miaka mingi.
Hatua
hizo zimefikiwa Ikulu, Dar es Salaam jana baada ya Marais Jakaya Kikwete
na Filipe Nyussi wa Msumbiji kukubaliana kufanyia marekebisho mkataba
wa masuala ya uhamiaji kati ya nchi hizo mbili kudumisha udugu, urafiki
na uhusiano wa kirafiki.
Makubaliano
hayo yalifikiwa baada ya viongozi hao wakuu wa nchi hizo kufanya
mazungumzo ya faragha kwa saa kadhaa Ikulu, na kisha Mawaziri; Jaime
Basilio Monteiro, wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe,
aliyemwakilisha Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe,
kusaini hati ya makubaliano hayo.
Mkataba
huo wa sasa wenye marekebisho katika maeneo matatu makuu, umeeleza pia
kuwa muda wa siku 30 uliokuwa ukitolewa na Msumbiji kwa watanzania,
kukaa nchini humo bila kulipia viza sasa umeongezwa na kuwa siku 90.
Kutokana
na matakwa mapya ya mkataba huo wa sasa, Membe alisema umeweka usawa wa
siku za kuishi kwenye nchi hizo mbili kwa raia wa Tanzania na Msumbiji,
tofauti na ilivyokuwa awali kwamba watanzania walipewa siku hizo kuwepo
bure kwenye nchi hiyo wakati raia wa Msumbiji waliweza kuishi kwa siku
90 bila kutozwa ada ya viza.
"Makubaliano
ya Marais hawa yameleta ahueni kubwa kwa raia wa nchi hizi mbili katika
masuala ya uhamiaji. Wanafunzi nao wamepata nafuu kubwa kwa sababu
hawataulizwa ada ya viza tena hadi wamalize masomo," alisema Membe.
Aliongeza
kuwa, mabadiliko hayo yanahusu hati za kidiplomasia, za kiserikali na
za kawaida ambapo, mtumiaji atagongewa viza bure kwa siku atakazo kaa,
ilimradi zisizidi 90.
Membe
alieleza kuwa kabla ya makubaliano hayo, raia wa Msumbiji alipaswa
kulipa ada ya viza ya Sh 10,000 tu, ili kukaa nchini kwa siku zisizo
zidi 90, wakati raia wa Tanzania aliyekwenda Msumbiji na kukaa kwa zaidi
ya siku 30, alipaswa kulipa Dola za Marekani 900 ikiwa ni ada ya viza.
Pia,
alibainisha kuwa, Mtanzania aliyekwenda nchini humo kwa shughuli za
biashara alipaswa kulipa ada ya viza ya Dola za Marekani 700, wakati
mfanyabiashara wa Msumbiji aliyekuja nchini kwa shughuli kama hizo
alitozwa ada ya viza ya Dola za Marekani 200 tu.
Rais
Nyussi aliingia nchini saa 6:00 mchana kwa kupitia Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Kikwete,
kabla ya kwenda Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa mapumziko mafupi
na baadaye Ikulu kwa mazungumzo yaliyo zaa makubaliano hayo.
Akiwa
uwanja wa ndege, Rais Nyussi alikagua gwaride la heshima, kupigiwa
mizinga 21 na kujionea ngoma ya asili ijulikanayo kwa jina mnanda.CHANZO: HABARI LEO
No comments:
Post a Comment