Viongozi
wa Afrika wameaswa kuhakisha kuwa wanaweka mbali uchu wa madaraka ili
wasiji kuzidumbukiza nchi zao katika vita na migogoro kama inavyotokea
huko nchini Burundi huku watanzania wakitakiwa kutambua kuwa amani
iliyopo nchini ni lazima itunzwe na kamwe wasidanganyike kuwa hali ya
amani iliyopo itaendelea kuwepo kama wataligawa taifa katika misingi ya
ukabila na udini.
Hayo yamesemwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa nchi huru za
Afrika Dk Salim Ahmed Salim na ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya
Mwalimu Nyerere wakati akifungua mkutano wa mashauriano kuhusu amani na
umoja wa nchi, mkutano uliohusisha viongozi wa dini, wazee, siasa na
wale wa vyama vya siasa.
Akizungumzia malengo ya mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na
mwenyekiti mtendaji wa makammpuni ya IPP Dk Reginald Mengi pamoja na
makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, mkurugenzi
wa taasisi ya Mwalimu Nyerere Mh Joseph Butiku amesema wameona ni busara
kukaa na kuona nini kifanyike kuinusuru amani ya nchi hii hasa katika
kipindi hiki ambacho inaonekana dalili za upotevu wa amani zimeanza
kuonekana waziwazi.
Akitoa salamu za wazee Brigedia Jenerali Fransis Mbena amesma ili
amebani iwepo lakixia wazee wa zamani na wa sasa watote wapewe hakili
sawa na siyio kubagua kwania kwa kufanya hivyo ni kudhofisha misingi ya
mani iliyopo.
Mkutano pia ulihudhuriwa na wenyeviti wa vyama vya siasa akiwemo
Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na mwenyekiti wa NCCR mageuzi James
Mbatia na pamoja na katibu mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa ambapo
wamesema serikali inapaswa kuweka wazi ratiba ya uchaguzi ili kuepusha
uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment