Zaidi ya wakazi elfu ishirini na tano na miatano wa kata ya manyoni wanakabiliwa na shida ya maji kufuatia maeneo yaliyo kuwa ya wazi na yenye visima vitatu vya maji ,kugawiwa baadhi ya wafanya biashara na kujenga nyumba za kulala wageni,jambo ambalo limekuwa likisababisha wakazi hao kufuata maji ya visima umbali mrefu ambayo siyo salama kwa matumizi ya binadamu.
Wakiuliza maswali ya papo kwa hapo katika kikao cha baraza la madiwani wilayani manyoni,diwani wa kata ya Rungwa Bwana Machapaa John na diwani wa kata ya Itigi majengo Bwana Hussein Simba, wametaka kufahamu kigezo kilicho tumika kugawa maeneo hayo yenye visima vya halmashauri,huku wananchi wakiachwa kuendelea kuwa na shida ya maji kwa muda wa miaka mingi.
Akijibu swali hilo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya manyoni Bwana Supert Mseya pamoja na kutoa notisi ya kubomolewa nyumba hiyo ya wageni ,lakini amekiri kuwa eneo hilo ni lawazi na lilikuwa na visima vya maji na kugawiwa watu bila utaratibu.
No comments:
Post a Comment