Wananchi katika kijiji cha MATEMANGA wilayani tunduru mkoani RUVUMA wanaishi kwa hofu na kulazimika kutotembea usiku wakihofia kuliwa na simba wanaosumbua katika kijiji hicho wakidaiwa kutoroka katika hifadhi ya taifa ya SELOU ambapo mpaka sasa wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini.
Wamesema simba hao wanaodaiwa kuwa watatu na wazee ambao ina daiwa wametoroka porini baada ya kushindwa kuwinda kutokana na uzee ambapo wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini kijijini hapo wamekuwa wakisumbua katika kijiji hicho nyakati za usiku na kuwafanya waishi kwa hofu wakihofia kuliwa na simba hao.
Mhifadhi wa wanyamapori katika wilaya ya tunduru Bw.Charles Shawa anasema kuwa msako mkali wa kusaka simba unaendelea huku akisema ni simba mmoja tu ndiye anayesumbua kijijini hapo.
Mkuu wa wilaya ya tunduru Bw.Chande Bakary Nalicho anasema nguvu zimeongezwa katika msako wa simba ambapo kuna askari wanyamapori sita katika msako wa simba.
No comments:
Post a Comment