Thursday 7 May 2015

Wananchi 6000 wakosa mawasiliano ya barabara na Umeme baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba Daraja.


Zaidi wa wananchi 6000 wa kata ya wazo jimbo la kawe na kata ya goba jimbo la ubungo jijini dar es salaam hawana mawasilaiano ya barabara na huduma ya UMEME baada ya mto Tegeta kufurika maji na kusomba daraja lao la muda walilokuwa wanategemea kuvukia na kusababisha shughuli za kata hizo kusimama.

Wakazi hao wamethirika zaidi kutokana na mto huo kufurika maji  huku ukiendelea kulika ukizifuata nyumba za wananchi na wakazi wa mtaa wa muungano waliopo kata ya goba na  mtaa wa kilimahewa waliopo kata wazo ambapo mwandishi ameshuhudia wakazi hao wakilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kutumia kamba kwa ajili ya kuvuka huku nguzo ya umeme mkubwa ikiwa inaninyinia katikati ya mto huo Jambo lilolazimu shirika la ugavi wa umeme nchini kakata huduma ya umeme katika kata hizo.
 
Wakizungumza na MBEYA LEO wakiwa wamefatana na mwenyekiti wao wa mtaa wa muungano wananchi hao wamewalaumu vingozi wao wakiwemo wabunge na viongozi wa wilaya ya kinondoni kwa kutowawekea daraja la kudumu katika mto huo na kuwasababishia adha kila mara mvua kubwa inaponyesha ikwemo ya mwaka jana.
 
Wakazi wengine waliokubwa na mafuriko ni wanaoishi kandokando ya mto mbezi ambapo nyumba zao zimesombwa na maji huku kingo za mto huo zikiendelea kulika na kufuata nyumba zao ambapo wameiomba serikali kuwapatia viwanja vya bei raisi sehemu nyingine. 
 
Katika tukio lingine mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha visima vya mafuta kujaa maji na kusababisha baadhi ya madereva wa vyombo vya moto  kukumbwa na adha kubwa ya magari yao kuzima baada ya kuwekewa mafuta yalichanganyika na maji ya mvua katika kituo cha mafuta  cha kobil kilichopo afikana huku meneja wa kituo hicho akisuasua kuwalipa madereva hao.

No comments: