Saturday 27 June 2015

Wakulima zaidi ya laki saba wanasadikiwa kuathirika na viwatilifu vyenye sumu katika mikoa mbalimbali Nchini.


Wakulima zaidi ya laki saba kutoka mikoa ya mwanza,mbeya,Kilimanjaro na Iringa wanasadikiwa kuathirika na viwatilifu vyenye sumu kali vinavyotumika kuua wadudu na magugu mashambani kutokana na ukosefu wa elimu ya kujikinga na matumizi ya  viwatilifu hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na kaimu msajili wa taasisi ya utafiti na udhibiti wa viwatlifu nchini –TPRI- Dokta Elikana Lekei wakati akitoa elimu juu ya matumizi bora ya kujikinga na madhara ya  viwatilifu kwa wakulima na wafanyabiashara wa dawa hizo katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara.
 
Amesema kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa mwaka 200-2006 katika mikoa hiyo imeonyesha madhara ya viwatilifu ni makubwa nchini na mkakati uliyopo hivi sasa ni kuangalia maeneo yenye athari kubwa ili wakulima wapimwe lakini pia wapewe ushauri utakaosaidia kuwapunguzia matatizo ya kiafya.
 
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakizungumzia hali hilo wamesema elimu hiyo imewawezesha kutambua madhara ya viwatilifu hivyo hasa vitumikavyo kwenye mmea wa mkorosho ambavyo vingi vinauzwa kiholela.

No comments: