MWALIMU mstaafu, Rashid Mbogo (65) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kupatikana hatia ya kumnajisi mjukuu wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa
alisema kuwa mahakama hiyo imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande
wa mashtaka na utetezi ambapo haukuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa
huyo alitenda unyama huo.
Hati ya mashtaka mahakamani hapo inaeleza kuwa mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo, Oktoba 19, mwaka jana, saa mbili na nusu usiku
nyumbani kwake kijijini Majalila wilayani humo.
Katika shauri hilo mshtakiwa hakuwa na shahidi ambapo upande wa mashtaka uliita mashahdi sita akiwemo mtoto wa mshtakiwa.
No comments:
Post a Comment