JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa
Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 08.05.2017.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye
tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio
makubwa ya uhalifu.
KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI
Mnamo
tarehe 06.05.2017 majira ya saa 21:30 usiku huko katika Kijiji cha
Mahongole, Kata ya Imalilo - Songwe, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa
wa Mbeya, Jeshi la Polisi lilifanya msako na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la MARIAM SIMON
[25] Mkazi wa Mahongole akiwa na vipande
19 vya nyama ya ngiri katika nyumba yake.
Mtuhumiwa
alikamatwa na nyama hizo baada ya kupekuliwa katika nyumba yake anayoishi
pamoja na mumuwe ambaye amefanikiwa kukimbia. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kuhusiana
na tukio hilo. Upelelezi unaendelea.
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
Mnamo
tarehe 07.05.2017 majira ya saa 13:00 mchana huko maeneo ya Forest,
Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi
lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye CALVIN
SHILONGI @ MAHEMBE [24] raia na mkazi wa nchini Botswana kwa kosa la
kuingia nchini bila kibali. Upelellelzi unaendelea.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linaongeza jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama katika kuzuia na
kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa
barabara wanatii, wanaheshimu na kufuata sheria za usalama barabarani. Aidha
kumekuwa na tukio 01 la ajali ya kifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 08.05.2017 majira ya saa 05:10 Alfajiri huko eneo la
Sokoine, Kata na Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya katika Barabara ya
Mafiati-Sokomatola, Gari yenye namba za usajili T.866 CGC aina ya Toyota Honda iliyokuwa ikiendeshwa na dereva
aitwaye FRANK MWAISANILA umri kati ya
miaka 25 - 30 Mkazi wa Isyesye iliacha njia, kupinduka na kusababisha kifo
kwa dereva huyo.
Aidha
katika ajali hiyo mtu mmoja ambaye alikuwa abiria katika gari hiyo aitwaye JOHN CHOGO [28] Mkazi wa Sokomatola
alijeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo alipatiwa matibabu na kuruhusiwa.
Chanzo
cha ajali ni mwendo kasi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa
Mbeya.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa
taarifa za siri kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka. Pia Kamanda
KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi
kuwa makini na watu wanaowatilia mashaka hasa wahamiaji haramu kwa kutoa
taarifa mapema ili upelelezi dhidi yao ufanyike.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A.
KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment