Mbunge
wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na
kutoa kauli yake baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia gharama za
matibabu ya Tundu Lissu popote duniani na kusema huo ni utani wa
serikali ya awamu ya tano.
Mbunge
Msigwa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kusema kuwa
serikali ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lissu popote duniani baada ya kupata maombi kutoka kwa
familia ya Tundu Lissu na kama ripoti ya madaktari itaonyesha kuna
ulazima kiongozi huyo kupatiwa matibabu zaidi basi serikali itasimamia
jambo hilo.
Kutokana na kauli hiyo Msigwa amedai huo ni utani wa serikali "Huu ni utani wa serikali ya awamu ya tano" alisema Peter Msigwa
Mbali
na hilo Mbunge Peter Msigwa alisema kuwa wao wanatambua thamani na
umuhimu wa Tundu Lissu na kusema kuwa wapo tayari kuuza vitu vyao
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anapata matibabu na
kurejea nchini akiwa salama.
No comments:
Post a Comment