Taasisi
tatu za juu za wanasheria za Uingereza zimeungana na kumwandikia barua
ya wazi Rais John Magufuli zikiomba mamlaka kufanya uchunguzi wa kina
juu ya tukio la kupigwa risasi kwa Lissu na kumfutia kesi zote
zinazomkabili ambazo zimekosa ushahidi wa kutosha.
Barua
hiyo imeandikwa juzi na kusainiwa na vigogo wa Chama cha Mawakili
Uingereza (LS), Kamati ya Haki za Binadamu ya Wanasheria Uingereza
(BHRC) na Baraza la Wanasheria (BC).
Vigogo
hao, Rais wa LS, Joe Egan; Mwenyekiti wa BHRC Andrew Langdon na
Mwenyekiti wa BC, Kirsty Brimelow wamesema wanaguswa na matukio
yanayoendelea dhidi ya Lissu ikiwamo ya matukio ya kukamatwa na polisi
na kufunguliwa mashtaka mara kwa mara huku pia ikiorodhesha matukio
mengine ya kihalifu yaliyowakumba wanasheria wengine likiwamo la
kulipuliwa ofisi ya kampuni ya uwakili ya Immma ya jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
Pia,
wamesema wameguswa na vitisho dhidi ya TLS kikiwemo cha kukifuta chama
hicho kilichotolewa na Dk Harisson Mwakyembe mapema Februari wakati
akiwa Waziri wa Katiba na Sheria iwapo ingeendelea kujihusisha na
“uanaharakati wa kisiasa.”
Kutokana
na mwenendo wa matukio hayo, barua hiyo inaomba ufanyike uchunguzi wa
kina na huru utakaoibua ukweli juu ya kupigwa risasi kwa Lissu na
matukio mengine ya uhalifu yaliyowakumba wanataaluma wengine wa sheria
na kuwachukulia hatua wote wanaohusika kwa mujibu wa sheria na taratibu
za kimataifa.
“Tunazisihi
mamlaka kumfutia mashtaka yote yanayomkabili Lissu vinginevyo kuwe na
ushahidi wa kutosha na uwe wa wazi na kuwe na fursa ya kukata rufaa,”
inasomeka sehemu ya barua hiyo na kuongeza;
“Tunaisihi
Tanzania kuheshimu matakwa ya kimataifa, iwalinde wanasheria ili
kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao vyema bila vitisho, vikwazo,
unyanyasaji wala kuingiliwa majukumu yao.”
No comments:
Post a Comment