Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kuwakamata watu wote waliohusika kuchakachua fedha za ujenzi
wa jengo la Zahanati ya Neruma.
Dk.
Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akiwa katika ziara yake ya
kuimalisha sekta ya afya wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo aliweza
kukagua jengo jengo la Zahanati ya Neruma,iliyopo Kata ya Neruma
Wilayani Bunda, Mkoani Mara na kubaini milioni 29 fedha za ujenzi zikiwa
zimechakachuliwa.
Akizungumza
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isaack Mahela alimweleza Naibu Waziri
kuwa, ujenzi wa jengo hilo umegharimu jumla ya milioni 29 kwa ajili ya
kupanua na kuweka fremu za milango pamoja na madirisha, kitu ambacho
kimeonekana hakiendani na uhalisia wa fedha hizo.
"Nakuagiza
Mkurugenzi, uhakikishe unawasilisha nyaraka zote za fedha za jengo hili
kwa TAKUKURU na wale wote waliohusika kupitisha fedha hizo na
uwakabidhi TAKUKURU ili wafanye uchunguzi na kuchukua hatua
zichukuliwe", amesema Dkt. Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla amesema kuwa taifa linataka kusonga mbele hivyo watu
wanaokwamisha mchakato wa Rais wa kuwaletea maendeleo wananchi wake
lazima wachukuliwe hatua ili watu wengine waogope kutafuna fedha za
umma.
Jengo
hilo ambalo pia limeonekana kuwa chini ya kiwango katika maeneo kuta
zake, mchakato wa ujenzi wa jengo ulianza tokea mwaka 2015 kwa nguvu za
wananchi na baadae Halmashauri ilitenga fedha za kumalizia mchakato
kiasi cha milioni 29, ambazo zimebainika kutafunwa na watendaji
waliokuwa wanashughulikia zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment