Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri ameviagiza vyombo vya Ulinzi na
Usalama Mkoani humo kuwasaka watu wote waliohusika katika jaribio la
mauaji ya watu wanne ambao walipigwa na kuwachoma moto katika kijiji cha
Mwanabondo, Wilayani Uyui Mkoani humo kwa tuhuma za ushirikina.
Mwanri amesema kuwa vitendo vya wananchi kuendelea kujichukulia sheria
mikono havivumiliki na havikubaliki hata kidogo kwa kuwa vyombo vya
sheria vipo ambavyo vinaweza kutekeleza majukumu yake.
Mkuu huyo wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa amesema licha ya tukio hilo kutokea lakini sio la kwanza hivyo
vyombo vya usalama lazima vihakikishe vinawatia nguvuni watu
wanaotekeleza matukio hayo.
Wakiongea wakiwa Hospitali Mkoani humo baadhi ya wahanga wa Tukio hilo
wamesimulia jinsi walivyotaka kuuawa na watu hao wasiojulikana ambao
walitokomea mara baada ya kushindwa kutekeleza azma yao.
No comments:
Post a Comment