Rais John Pombe Magufuli ambaye leo Septemba 20, 2017 yupo kwenye ziara
ya kikazi mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro amefunguka na
kumsifia Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya na kusema ni mbunge
mchapakazi.
Rais Magufuli amesema Ole Millya ni mchapakazi kutokana na ukweli kwamba
mbunge huyo amelelewa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukulia
ndani ya chama hicho hivyo sasa yupo CHADEMA lakini moyo wake ni CCM.
"Miliya ni mchapakazi, kwa sababu amelelewa na CCM, unaweza kumuona ni
CHADEMA lakini moyo wake huyu ni Chama Cha Mapinduzi (CCM)" alisema
Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa Mungu huenda alikosea kuipa
Tanzania madini ya Tanzanite kwani madini hayo yamekuwa yakiibiwa huku
Watanzania wenyewe wakishindwa kunufaika na mapato ya madini hayo.
"Mungu alifanya makosa alileta Tanzanite kwa Watanzania, lakini kama
hakufanya makosa basi tubadilike jinsi ya kutumia Tanzanite. Tanzanite
ingekuwa inatumika vizuri kusikungekuwa na tatizo la barabara hapa
Simanjiro, hapa Simanjiro msingekosa hata Ambulance moja lakini kwa kuwa
hamna gari hata moja ya wagonjwa basi mimi nitaleta gari ya wagonjwa
hapa nitajua nifanya nini, nitawakata kata huko tutapata gari" alisema
Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment