Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amepandishwa kizimbani leo
Alhamisi katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na
kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.
Mbali
na Msigwa pia Diwani wa Viti Maalum, Selestina Johanes na dereva wa
mbunge huyo, Godi Mwaluka wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo.
Akisoma
shtaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Rehema Mayagilo amesema kuwa
mbunge huyo na washtakiwa hao wawili wanashtakiwa kwa madai ya kumtusi
na kutishia kumuua diwani huyo.
Hakimu
Mayagilo amesema kuwa Msigwa na wenzake walitenda kosa hilo jana saa
nane mchana katika viunga vya Ofisi za Halimashauri ya Manispaa ya
Iringa.
Baada
ya kusomewa shtaka hilo Msigwa na wenzake wamepata dhamana na kesi hiyo
imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment