Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ameagiza Jeshi la Wananchi kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta mkubwa
kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite na kuweka mitambo maalum, ili
kulinda madini hayo yasiendelee kuibiwa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
ambako ameende kuzindua barabara ya lami iliyojengwa kwa bilioni 32.5 ya
KIA- Manyara, na kusema kwamba ni lazima ulinzi huo uwekwe ili kuokoa
rasilimali za Tanzania zisiendelee kuibiwa na nchi kubaki masikini.
"Eneo la Simanjiro kuanzia Block A mpaka Bolock D ambalo lina madini
mengi, ninaagiza Jeshi la wananchi likishirikiana na Suma JKT, waanze
kulijengea ukuta eneo lote, wataweka fensi juu na wataweka camera,
patawekwa mlango mmoja na itawekwa mitambo maalum, hata kama utameza
Tanzanite itaonekana, hata ukificha kwenye kiatu itaonekana", amesema
Rais Magufuli.
Rais Magufuli atakuwepo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3,
ambapo pia atatoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi
katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Septemba 23, 201
No comments:
Post a Comment