Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga
imewahukumu ndugu sita wa familia moja kunyongwa hadi kufa baada ya
kutiwa hatiani kwa kumuua kwa kukusudia ndugu yao Raymond Kamande
wakimtuhumu kuwa mchawi.
Wanandugu hao ambao ni wakazi wa kijiji
cha Mkoe wilayani Kalambo wanadaiwa usiku huo wa tukio wakiwa na fimbo,
fyekeo, mapanga na mashoka walivamia na kuteketeza nyumba ya ndugu yao
huyo kwa moto kisha wakamuua na mwili wake wakauchoma moto.
Waliohukumiwa kifo na mahakama hiyo ni
pamoja na Peter Mpandashalo, Aristed Kamande, Stephan Sikanda, Herric
Nguvumali na Anatory Kamande. Aidha mahakama hiyo iliwaachia huru ndugu
wawili Wilbroad Kamande na Aristed Kamande.
Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama
hiyo, Dk Adam Mambi alisema washitakiwa hao sita walitenda kosa hilo
kinyume na kifungu 199 cha makosa ya jinai Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
mapitio mwaka 2002.
Upande wa mashtaka uliongozwa na Wakili
wa Serikali, Scholastica Lugongo akisaidiwa na Adolf Lema waliwaita
mashahidi sita kuthibitisha bila kutia shaka ushahidi wao dhidi ya
uhalifu uliofanywa na washtakiwa.
Awali wakili wa serikali, Lugongo
alieleza mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda makosa
hayo Septemba 27, mwaka 2014 katika kijiji cha Mkoe wilayani Kalambo.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa usiku huo
wa tukio washtakiwa hao sita wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumba
ya ndugu yao Raymond kijijini hapo akiwa amelala humo na kuiteketeza kwa
moto.
Kwa mujibu wa Wakili Lugongo, Raymond
katika jitihada za kujiokoa alipenya kwenye dirisha la chumba chake
lililoanguka na kukimbilia kujificha kwenye nyumba ya mtoto wake wa
kiume, David Kamande.
IMEANDIKWA NA PETY SIYAME, SUMBAWANGA
No comments:
Post a Comment