Vijana wawili wanaosadikiwa kuwa wanajihususha na kuwateka waendesha
bodaboda Mkoani Tabora wameuawa na wananchi wenye hasira baada ya
mwendesha pikipiki kupiga kelele akiomba msaada alipokuwa amekabwa na
wezi hao kwa lengo la kumpora pikipiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora, Kamishina Msaidizi Mwandamizi Willibrod
Mtafungwa amemtaja kijana aliyekuwa amekodiwa na vijana hao na kuwabeba
kwa mtindo wa mshikaki, kwa jina la Haruna Bungala ambaye alikodiwa
majira ya saa nne eneo la shule ya msingi Kitete ambapo walimpeleka kata
ya Malolo na kuanza kumkaba.
Aidha kijana huyo Bungara ambaye alijeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali
kwenye shavu la kushoto amesema kuwa kama si kupiga kelele alikuwa
anauawa na waporaji hao lakini wananchi walijitokeza na kuanza kutoa
adhabu hadi kifo na kuchomwa moto,
Kwa upande wa Mwenyekiti wa waendesha bodaboda amewapongeza wanachi kwa kutekeleza adhabu hiyo dhidi ya waporaji hao.
No comments:
Post a Comment