Mbunge
wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefunguka
na kusema kuwa amepata taarifa jeshi la polisi linamtafuta na kusema
endapo jeshi la polisi litamwita kwa kufuata utaratibu basi na yeye
ataitika wito huo ila si kuviziwa
Mbunge
Msigwa ametoa taarifa hii kufuatia kuwepo kwa taarifa toka jana kuwa
kiongozi huyo naye anatafutwa na jeshi la polisi akidai kuwa ni moja
kati ya watu waliokuwa wakiratibu mkusanyiko wa maombi ambao ulitakiwa
kufanyika jana kumuombea Mbunge Tundu Lissu katika viwanja vya TIP Sinza
jambo ambalo yeye mwenyewe alipinga na kusema bado yupo nchini Kenya.
"Nimepata
taarifa Kuwa polisi wamenitafuta toka asubuhi (jana) maeneo ya sinza,
Wakisisitiza kuwa nipo hotelini hapo , wakati mimi niko Nairobi,
nitaitika wito wa polisi ukiletwa rasmi, sihitaji kuviziwa +255754360996
mnaweza kunipigia au kunitumia ujumbe mfupi Whatsaap" alisema Msigwa.
Mbunge
Peter Msigwa bado yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwenye matibabu ya
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi
na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment