Mbunge
wa Arusha Mjini ambaye sasa yupo nchini Kenya amewaomba Waziri wa Mambo
ya Ndani na IGP Sirro wawaachie watu ambao jana walikamatwa na jeshi la
polisi wakiwa wamevaa Tshirt za Tundu Lissu na UKUTA na kusema kitendo
hicho kinazidi kuleta chuki.
Lema
amesema hayo kupitia mitandao yake ya kijamii na kudai kuwa watu ambao
wameratibu maombi kwa ajili ya Tundu Lissu hawakupaswa kukamatwa bali
walipaswa kulindwa na jeshi la polisi kwani wao wanaratibu watu waweze
kumlilia Mungu wao kwa maombi na si vinginevyo.
"Hivi
kweli hawa watu wangekuwa wanafanya mkusanyiko wa maombi kwa ajili ya
Rais Magufuli au kiongozi mwingine yoyote yule hawa watu wangepata
mateso makubwa kama ambavyo wale vijana wamepata
"
Mwigulu Nchemba wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Kamanda Sirro
tunakuomba sana waachie watu wote waliokamatwa wakiwa wamevaa Tshirt za
UKUTA, waachie kwa sababu hiki mnachokifanya kikiendelea kukomaa siku
moja hamtawaona na Tshirt wala na kitu chochote wakiacha kuvaa Tshirt
mioyo yao ikaendelea kuumia wakiacha kusali maana yake watakuwa
wameelekea katika njia nyingine mbaya zaidi" alisisitiza Gobless Lema
Godbless
Lema ametoa kauli hii siku moja baada ya jeshi la polisi kuzuia watu
kufanya maombi ya kitaifa kwa Mbunge Tundu Lissu maombi ambayo
yaliandaliwa na vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ambayo yalipaswa kufanyika
Septemba 17, 2017 katika viwanja vya TIP Sinza Darajani.
No comments:
Post a Comment