Kesi namba 214 nayowakabili
Rais wa Simba, Evans Aveva nA Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu'
imetajwa tena kwenye mahakama ya hakimu mkazi kisutu mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Victori Nongwa.
Katika
kesi hiyo ambayo leo iliitwa kwa ajili ya kitajwa ambapo upande wa
uendesha mashitaka uliowakilishwa na wakili wa serikali Nassor Katuga
akisaidiwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
'Takukuru', Peter Vitalis.
Katuga
ameimbia mahakama hiyo kuwa tayari wameshakamilisha upepelezi wa kesi
hiyo na wamepeleka jarada kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP), kwa
ajili ya kupitia upelelezi huo ili kuona kama umekamilika kabla ya hatua
nyengine kuendelea.
Kutokana na hivyo, hakimu Victoria Nongwa ameharishia kesi hiyo hadi Septamba 27, mwaka
huu itakapotajwa tena mahakamani hapo baada ya kueleza upande wa
utetezi uliowakilishwa na wakili, Philemon Mutakyemirwa akisaidiwa na
Evodious Mtawala.
No comments:
Post a Comment