Askari
Polisi Stephen Mungai Kinuthia wa jimbo la Nakuru nchini Kenya,
amemuuwa mkewe kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kujiua mwenyewe
mbele ya mtoto wao ambaye alishuhudia tukio zima.
Kinuthia
ambaye alikuwa skari polisi wa kituo cha Molo, amempiga risasi mpenzi
wake huyo mara tatu kwa kutumia bunduki ya AK47 wakiwa nyumbani kwao.
Shuhuda
wa tukio hilo ambaye ni mlinzi wa eneo hilo amesema walisikia kelele za
watu wakilumbana, na walipokuwa wakikimbilia kujua kulikoni walisikia
milio ya risasi na kisha kukawa na ukimya.
Majirani wa eneo hilo wamesema walisikia kelele za mtoto akilia kwa sauti huku akisema baba anamuuwa mama.
OCPD
wa Nakuru Joshua Omukatta amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo, huku miili ya marehemu wote ikiwa imepelekwa katika hospitali ya
serikali ya Nakuru.
No comments:
Post a Comment