Serikali
kupitia wakala wake wa ujenzi nchini (TBA) imetoa msaada wa nyumba kwa
askari polisi waliounguliwa nyumba zao hapo jana, mpaka pale
watakapopata makazi rasmi.
Taarifa
hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,
ambapo amesema baada ya ajali hiyo askari hao walikosa mahali pakuishi,
hivyo wanaishukuru TBA kwa msaada huo.
"Ule
moto umeteketeza kila kitu kabisa, hivyo wale askari hawakuwa na sehemu
ya kuishi, jana tuliwahifadhi kwenye bwalo letu la polisi, lakini leo
wamepatiwa msaada na wakala wa ujenzi wa serikali (TBA ), wamepewa
nyumba za kuishi kwa muda hadi pale watakapopatiwa makazi rasmi,
tunashukuru kwa hilo", amesema Kamanda Mkumbo.
Tukio
la kuteketea kwa nyumba hizo limetokea usiku wa Septemba 27 mwaka huu
majira ya saa mbili na kuteketeza nyumba hizo, lakini jeshi la zimamoto
liliwahi eneo la tukio na kutoa msaada kwa wananchi ambao walianza
kuzima.
No comments:
Post a Comment