Ikiwa
ni siku tano tu zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area
D, Dodoma, tukio lingine kama hilo limetokea Dar es Salaam ambapo watu
wanaodhaniwa kuwa majambazi wamemshambulia kwa risasi Meja Jenerali
Vincent Mritaba.
Tukio
hilo limetokea jioni ya September 11, 2017 wakati Meja Jenerali Mritaba
akiwa anaingia getini nyumbani kwake Tegeta ambapo alivamiwa na watu
wasiojulikana na kupigwa risasi tumboni, begani na mguuni.
Hadi usiku wa jana Madaktari walikua wanaendelea na upasuaji kutoa risasi tatu tumboni na kushughulikia majeraha mengine.
No comments:
Post a Comment