Mwili
wa mtoto ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa siku moja umeokotwa kwenye
mfereji wa kupitisha maji machafu katika eneo la Mtaa wa Ali Nyanya kata
ya Ungalimited jijini Arusha.
Kichanga
hicho kimeonekana kutekelezwa na mama yake mzazi mara tu baada ya
kujifungua na kupelekea kupoteza maisha, baadhi ya wananchi wa eneo hilo
wamelaani kitendo hicho cha kinyama na kikatili kinachofanywa na baadhi
ya wanawake wasiokuwa na hofu ya Mungu ndani yao ambao wanakatisha uhai
wa watoto hao ambao hawana hatia.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo Omari Shehe naye amelaani kitendo hicho na kuahidi
kushirikiana na vyombo vya dola kuhakikisha wanamtafuta muhisika ambaye
amefanya tukio hilo la kinyama ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye
tabia hizo za kufanya uovu na ukatili huo.
Vitendo
vya watu kutekeleza watoto vimekuwa vikishamiri katika maeneo
mbalimbali ya nchi huku wengi wakionekana kufanya ukatili huo kutokana
na baadhi ya wanaume kukataa watoto au ujazito jambo ambalo hata hivyo
halikubaliki.
No comments:
Post a Comment