Mkuu
wa Shule ya Sekondari Migukulama iliyopo Halmasahauri ya Buchosa
wilayani Sengerema, Benerdicto Lweikiza (45) amejinyonga hadi kufa akiwa
chumbani kwake.
Taarifa
za kujinyonga kwa mwalimu huyo zilianza kusambaa wilayani Sengerema na
kuthibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Buchosa,
Crispin Luanda.
“Ni
kweli mwalimu huyo amejinyonga alikuwa mkuu wa Shule ya Sekondari
Migukulama na amefikia uamuzi huo majira ya saa tisa mchana wa leo
(jana) nyumbani kwake Mtaa wa Kilabela mjini Sengerema,” alisema Luanda.
Mmoja
wa wanafamilia wa mwalimu huyo, Martin Kalemera alisema kuwa wao kama
familia wanashangazwa na suala hilo na hawaamini kilichotokea ikiwa ni
miaka mitano imepita tangu mke wake afariki dunia.
Mkuu
wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alithibitisha kupata taarifa ya
kifo cha mwalimu huyo na kusema kuwa hajafahamu chanzo cha kufikia
hatua ya kujinyonga na kamba chumbani kwake.
Alisema vyombo vya dola vinafuatilia kwa kina ili kubaini sababu.
Tukio
hilo lilitokea saa chache baada ya gari aina ya Toyota Hiace kutumbukia
ndani ya Ziwa Victoria na kuua zaidi ya watu 12 katika eneo la Kivuko
cha Kigogo wilayani Misungwi.
No comments:
Post a Comment