Sakata
la wakimbizi kurudi nchini mwao ambalo limeendelea kubadilishwa
badilishwa kimtazamo na baadhi ya mashirika ya kimataifa, limetua kwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliyesisitiza kuwa
halijasitishwa.
Nchemba
amesema kazi ya kuwaandikisha wakimbizi wa Burundi wanaotaka kurejea
kwao kwa hiari haijasitishwa licha ya baadhi ya mashirika ya kimataifa
kudai usalama wa wale wanaorudishwa uko hatarini.
Hivi
karibuni shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty
International lilidai kwamba mpango wa kuwarejesha wakimbizi hao
unahatarisha maisha yao na linaamini kuwa wengi wanarejeshwa kutokana na
msukumo wa ushawishi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi.
Shirika
hilo lilidai kuwa hali ya usalama bado si shwari likieleza kuwapo kwa
matukio ya utesaji, kufungwa bila makosa, kubakwa na hata kuuawa.
Hata
hivyo, Mwigulu alionyesha kushangazwa na ripoti hizo akisema
mawasiliano yake na waziri mwenzake wa Burundi yamethibitisha kutokuwapo
kwa matukio ya aina hiyo.
“Sijui
hizi ripoti wanazipata wapi, mimi nimezungumza na mwenzangu wa Burundi
na amenithibitishia kuwa hali iko shwari na hakuna dhoruba zozote
zinazowapata wakimbizi wanaorejea kwao.
"Wakimbizi
wanaojiandikisha wameongezeka mara mbili kuanzia wale wa awali 12,000
na sasa wamefikia 24,000. Hawa wakimbizi wamethibitishiwa na ndugu zao
kuwa hali nyumbani kwao ni shwari na ndiyo maana wanaendelea
kujiandikisha,” alisema.
Mwezi
uliopita, Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa
linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) walikubaliana kuwa ifikapo mwishoni mwa
mwaka huu wawe wamewarejesha wakimbizi 12,000 wanaoishi Tanzania ambao
wanataka kurudi kwao Burundi kwa hiari.
No comments:
Post a Comment