Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Geita, Joseph Kasheku Msukuma
amesema kuwa endapo watashinda kesi dhidi ya mgodi wa GGM ambayo
wameifungua, watakuwa na uhakika wa kupata fedha ambazo zinaweza
kuhudumu katika halmshauri kwa miaka 29, bila kuomba kwa Rais fedha
yoyote.
Msukuma
ambaye pia ni Mbunge wa Geita amesema hayo alipokuwa kwenye uchaguzi wa
Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya ya Geita ambapo alitumia nafasi hiyo
kuwataka madiwani wa CCM wote ambao wanahitajika kituo cha polisi waende
polisi wenyewe wakahojiwe na kuwaambia siku ya kwenda mahakamani wavae
sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nitumie
fursa hii kuwaomba madiwani wote wa CCM wa Geita Mjini, Geita na wale
wa Busanda ambao tulikuwa kwenye kikao kile jitokezeni, muende wenyewe
polisi, msikimbie nendeni wote polisi na tarehe 9 na 10 tunaenda
mahakamani na sare za CCM, na mimi kamanda wenu nawaambia kuwa
tutashinda tumeweka mawakili tisa. Dola milioni 12 ni sawa na bilioni
29, halmashauri kama ya Geita peke yake huwa tunatumia bilioni 1.5 mpaka
1.8 maana yake wakitulipa hizo hela tunaweza kuwa na miaka 29 bila
kumuomba Rais hela,”alisema Msukuma.
Mbunge
Msukuma pamoja na madiwani kadhaa wa CCM waliingia katika misukosuko
wiki kadhaa zilizopita baada ya kukamatwa na jeshi la polisi na kulazwa
ndani kwa masaa 24 kwa kile kilichoeleza kuwa walihusika katika kufanya
vurugu kwenye mgodi wa Geita Gold Mine na kufunga barabara inayoingia
mgodini huko wakishinikiza malipo hayo ya Dola milioni 12.
No comments:
Post a Comment