Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM, Hamphrey Polepole amesema mchakato wa Katiba
ulikwama kwa sababu hakukuwa na uelewa wa pamoja nini wananchi wanataka
jambo ambalo, tayari limeshaeleweka ndani ya chama hicho.
Akizungumza
leo Alhamisi katika kipindi cha Maisha Mseto kinachorushwa na redio
Times FM, Polepole amesema yeye ni muumini wa maoni ya wananchi kwenye
mchakato wa Katiba mpya.
Amesema
wakati ya mchakato wa Katiba mpya alikuwa miongoni mwa wajumbe
waliokusanya maoni ya wananchi ataendelea kuunga mkono maoni yao.
“Nilikusanya
maoni ya wananchi nchi nzima ya Tanzania na ninajua nini Watanzania
wanasema kwa hiyo, mimi ni muumini wa maoni ya wananchi,” amesema.
Amesema mchakato huo ulikwama kwa sababu hakukuwepo na uelewa wa nini Watanzania wanataka.
Hata hivyo alidai kuwa mabadiliko makubwa yanayofanywa ndani ya chama hicho yanaakisi kushughulikia kero za wananchi.
“Siasa
safi ni kushughulika na kero za wananchi wetu, chama kimejitathmini na
kujisahihisha kwa sababu tumepata usahidi kwamba kuna mahali tulikosea
kwa hiyo, tunao utaratibu wa kujikosoa,” amesema.
Polepole
amesema uongozi wa Rais John Magufuli umejikita zaidi katika
kushughulikia kero za wananchi kwa kuhakikisha watumishi wa umma
wanafanya kazi kwa uadilifu huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa.
No comments:
Post a Comment