Rais
John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia juu ya ndege za Tanzania
sita zilizonunuliwa na serikali ikiwepo Bombardier Q 400-Dash ambayo
inashikiliwa nchini Canada na kusema ndege hizo zitawasili nchini
mwakani 2018.
Rais
Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya
Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu
Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa
watalii wengi kutokana na kukosa ndege.
"Tumenunua
ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine
ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni. Tunafanya haya kwa
ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi
ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya
pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii
wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais Magufuli
Serikali
ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8 iliyonunuliwa na
serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi Julai lakini
ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil
Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400-Dash 8
iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.
No comments:
Post a Comment