Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi
kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri wanne kwa ulevi wa pombe
pindi wawapo makazini.
Rais
Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya
Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mwalimu Nyerere Dar es Salaam na kusema amepata taarifa kuwa wapo
Wakurugenzi kadhaa ambaio ni walevi na kudai wasipobadilika ndani ya
muda mfupi atawafukuza kazi.
"Nimepata
taarifa ya Wakurugenzi kama wawili watatu hivi ni walevi sana,
nawaambia hao wataondoka kama upo hapa Mkurugenzi halafu ni mlevi
ukajirekebishe haraka sana, kabla sijaja huko ili angalau uonekane
umebadilika" alisema Rais Magufuli.
Mbali
na hilo Rais Magufuli aliwataka viongozi hao kwenda kumaliza migogoro
mbalimbali ndani ya halmashauri zao na mivutano isiyokuwa na msingi na
kusema kuwa vyama vya siasa si adui bali adui wa kwanza wa serikali yake
ni watu wanaokuja kuiba maliasili za Tanzania.
"Haipendezi
kuwa na makundi, muyamalize makundu hayo kwenye manispaa, tunajenga
nyumba moja adui yetu siyo vyama tunachelewa sana, adui yetu ni wale
wanaotuibia nasema mkamalize hayo makundi huko, najua tofauti lazima
zitakuwepo lakini kwenye masuala ya kazi lazima tushikamane kwa maslahi
ya Watanzania, mkawaimize Watanzania kufanya mambo ya maendeleo"
alisisitiza Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment