Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za kampuni ya mfanyabiashara Yusufu Manji kutokana na kudaiwa Sh 12.2 bilioni.
Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo amesema wamekuwa na
mawasiliano na kampuni ya Farm Equpment ambayo inamilikiwa na Manji
tangu Agosti 15 mwaka huu lakini kulikuwa hakuna mrejesho kuhusu deni
hilo.
Kutokana
na hilo amesema wamefunga ofisi zake kwa sababu kampuni hiyo inadaiwa
kiasi cha Sh 12.2 bilioni lakini kampuni hiyo ina nafasi ya kuendelea
kuwasiliana na TRA namna ya kulipa deni hilo.
Tukio
hilo limetokea leo Jumatatu kati ya saa 4 hadi 7 wakati TRA na kampuni
ya udalali ya Yono wakiambatana na polisi walipokwenda katika jengo hilo
lililopo barabara ya Pugu, wilayani Temeke.
Baadhi
ya mashuhuda wakiwamo walinzi kwa masharti ya kutotaja majina yao
wamesema kuwa ofisi zilizofungwa ni ya Manji na sehemu yake duka la
kuuza pikipiki na matrekta.
Wamesema
baada ya kufika watu waliingia moja kwa moja katika ofisi yake kisha
kufanya majadiliano na wahusika yaliyodumu zaidi ya saa 2.
"Nadhani
hawakufikiana mwafaka kwa sababu walivyotoka wakaamuru wafanyakazi wa
ofisi hiyo kutoka nje kisha kuweka utepe wa rangi nyekundu na nyeupe,"
amesema shuhuda huyo.
Hata
hivyo, mashuhuda hao wamesema hawajui tatizo ni nini lakini waliwasikia
maofisa wa TRA na kampuni hiyo ya udalali wakizungumza kuhusu kodi.
No comments:
Post a Comment