Vigogo wawili wa chuo cha uhasibu (TIA) jijini Dar es Salaam, leo
wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu
mashtaka mawili, la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia
serikali hasara ya zaidi ya bilioni moja.
Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali kutoka Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa, Leornad Swai amewataja watuhumiwa hao kuwa ni,
Shaha Mussa Hanzuruni na Onesphory Ambangile Luhungu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba imedaiwa, kati ya January Mosi
2012 na Desemba 30 2014, katika chuo hicho cha TIA kilichopo katika
wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam washtakiwa hao walitenda kosa la
matumizi mabaya ya madaraka.
Imedaiwa, washtakiwa, walitumia vibaya madaraka yao kwa kutofuata
taratibu za manunuzi katika ununuzi wa ardhi wa chuo hicho (TIA) kampasi
uya Mwanza na kimsababishia Vedasto Lupungo kupata manufaa ya
Sh.1,097,681,107./-
Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa
ridhaa zao na matendo yao waliisababishia TIA Hasara ya Sh.
1,097,681,107/- kwa kutokifuata sheria za manunuzi wakati wa kusaini
mkataba wa ardhi wa eneo la TIA kampasi ya Mwanza.
Kwa kuwa DPP ameipa mamlaka mahakama ya Kisutu kisikiloza kesi hiyo ya
uhujumu uchumi, washtakiwa walipata nafasi ya kijibu juu ya tuhuma hizo
ambapo wote wamekana kutenda makosa hayo na mahakama ikawasomea masharti
ya dhamana kwa kuwa kesi hiyo inadhaminika
Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Simba amewata washtakiwa kuwa na
wadhamini wawili watakaoweka bondi ya milioni 250 kila mmoja, pia
amemtaka mdhamini mmoja kati ya hao kuweka mahakamani pesa taslimu,
milioni 250 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho
cha fedha ambayo Ipo ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
Pia wametakiwa kuwasilisha Pasi zao za kusafiria vilevile hawaruhusiwi
kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ruhusa ya maandishi kutoka
mahakamani hapo.
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment