Monday, 19 January 2015

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YATOA UFAFANUZI WA SINTOFAHAMU UKARABATI WA BARABARA YA IGANZO- KABWE.


Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akizungumza na vyombo vya habari Iganzo jijini Mbeya kuhusiana na ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe.

Mhandisi Msaidizi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Injinia Chaula, ambaye ndiye anayesimamia barabara hiyo akionesha namna Greda linavyopasa kusembua kifusi kabla ya kushindilia.

Afisa Mstaafu wa Idara ya ujenzi mkoani Mbeya,Betwel Mbelile akionesha kushangazwa na namna barabara hiyo inavyokarabatiwa.


Sehemu ya barabara ambayo imekamilika baada ya kumwagwa kifusi na kushindiliwa tayari kwa kuanza kutumika.


UONGOZI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya umelazimika kutoa ufafanuzi wa sintofahamu kuhusu ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi.


Baadhi ya Wakazi wa Isanga walitoa malalamiko yako kwa vyombo vya habari wakilalamikia hatua zilizocghukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuamua kukarabatio Barabara ya Iganzo- Kabwe kwa kufukia vifusi vya mawe juu ya Lami huku wakihofia mvua zinazonyesha kuweza kuharibu.


Kutokana na malalamiko hayo na kuripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari baada ya uongozi wa Jiji kushindwa kujitokeza ili kuyatolea ufafanuzi ndipo Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akalazimika kufika eneo la mradi na kuzungumza na vyombo vya habari.


Mhandisi Sanya alisema ukarabati unaofanyika katika barabara hiyo ni kwa ajili ya kupitika katika kipindi kifupi wakati Uongozi wa Jiji ukijipanga kufanya ukarabati mkubwa hivyo kulazimika kuziba kwenye sehemu zilizokuwa zimechimbika sana huku sehemu nzuri zikirukwa.


Alisema baada ya kifusi kumwagwa Greda hupita na kuvuruga sehemu ya Lami ilichini ikichanganya na kifusi kisha kushindiliwa vizuri hali itakayosaidia njia hiyo kupitika kirahisi na kurahisisha masuala ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.


Aliongeza kuwa mbali na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kukosa fedha za kujenga upya barabara hiyo pia ikio kwenye mazungumzo ya kuifanya Barabara hiyo kupandishwa hadhi na kuwa ya Mkoa.


Akizungumzia kuhusu vifaa na Ukandarasi alisema kazi hiyo inafanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufuata kanuni za manunuzi ya umma isipokuwa Vifaa vilikosekana na kulazimu kukodi kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Communications Contractor Company Ltd(CCCC) na kufanya jumla ya gharama zote kufikia shilingi Milioni 37.

No comments: