Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesemasema kuwa imeridhishwa na maonyesho ya madini ya vito yaliyoandaliwa na jumuia ya wafanyabiashara wa madini nchini Tamida,kutokana na kuonyesha mafanikio makubwa yakiongozwa na madini ya Tanzanite.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simba Chawene,ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua maonyesho ya nne ya madini ya vito yanayoshirikisha wauzaji, wanunuzi wakubwa wa madini hayo ulimwenguni .
Chawene,amesema kuwa hivi sasa serikali ipo katika hatua za uimarishaji wa kiutengenezaji madini ukataji wake na uchongaji hivyo kuyauza yakiwa yameongezewa thamani na kutoa ajira nyingi tofauti na awali ambapo yalikuwa hayatoi ajira hizo kutokana na kuuzwa yakiwa ghafi.
Amongeza kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kutengeneza kituo kikubwa cha kuuzia madini ambapo kutakuwepo na Hotel, maduka na ofisi za mamlaka ya mapato TRA, na uwanja wa kutua Helkopta na hivyo kuondoa ulanguzi wa madinin na hivyo kuongeza pato la taifa sanjari na kuondoa urasimu uliokuwepo wakati wa mauzo ya madini.
Pia serikali itaweka vituo maalumu vya ukaguzi kwenye machimbo ya Tanzanite,ili kudhibiti wizi sanjari na kurejesha utaratibu wa kujenga ukuta uliokuwepo kwenye machimbo hayo ambao ulibomolewa na baadhi ya watu wenye nia mbaya ili waweze kutorosha madini hayo kwa urahisi ,pia kuimarisha ,utolewaji wa vitambulisho .
Ameongeza kuwa utoroshaji wa madini unaofanywa na watanzania ambao wamepewa leseni za kuuza na kununua madini umepungua kutokana na udhibiti kuimarishwa.
Amesem,a miaka miwili iliyopita Tanzania ilipata dola milioni 38 za kimarekani kutokana na mauzo ya Tanzanite, huku Kenya ikipata dola milioni 100 kutokana na mauzo ya Tanzanite, na India ilipata dola milioni 300.(Muro)