Sunday 19 April 2015

SOMO LA LEO: UNAWEZA KUAMUA KUWA NYUNDO AMA MSUMAR




Kila jambo lolote kwenye maisha ni maamuzi na kufwata kanunu sahihi juu ya kile ulichomua ndipo unaweza kuona unapiga hatua moja kwenda nyingine.Maamuzi ni kama alama ya kidole ya mtu(finger print) ambayo inaweza kumtofautisha kati ya mtu mmoja na mwingine.Kila matokeo unayoyaona leo kwenye jambo fulani ni kwamba mtu fulani aliamua kwamba jambo fulani litoke na akafwata kanuni kamili ndipo likatokea kwenye eneo husika.Maamuzi yanaweza kuboreshwa au yanaweza kuuchwa pia kama yalivyo.Iwapo unatamani kuwa mtu mwenye kiwango cha juu cha maamuzi mbali mbali amua kuboresha namna na kanuni ambazo unatumia kufanya maamuzi.

Mara nyingi kwenya maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiamuliwa mambo mengi na vitu mbali mbali badala ya sisi wenyewe kuwa chanzo cha maamuzi mbali mbali.Maisha yetu ya kila siku yamekuwa kama mkondo wa maji , ambayo huwa hayaulizi maswali zaidi kufwata njia ambayo imechongwa na maji yaliyopita wakati uliopita.

Unaweza ukaamua leo kuwa Nyundo kwenye kufanya maamuzi mbali mbali au unaweza kuamua kuwa msumari ambaye hutegemea nyundo ameamua nini leo?

Watu wengi tumekuwa waathiri wa maamuzi ya watu wengine bila sisi wenyewe kujua na huwa hatujiulizi kwanini ipo hivyo na je nini cha kubadilisha ili niweze kuvuka kutoka kwenye kuathiriwa na maamuzi ya mtu mwingine.Hakuna kitu kibaya zaidi kwenye maisha kama kulalamika ,malaliko yasiokuwa maamuzi sahihi huzaa Uchungu na baada ya kuzaa Uchungu huzaa Hasira na Hasira inapozaliwa Hali ya Kuona Unaonewa Huingia Moyoni na Hali Hiyo ikiingia mwisho wa siku Uasi hungia na Uasi Ukiingia ,Mwisho wa Siku majuto huwa kwa kiasi kikubwa sana

Hakikisha kila siku unajenga uwezo wa kuboresha maamuzi yako kwa kujifunza vitu kadha wa kadha kuondoka na kongwa la kuwa msumari na baada yake uwe nyundo.Nyundo anapoaamua kugonga msumari haulizi kama msumari ana umia au hapana.Msamuri ndiye anayeona maumivu ya kugongwa na nyundo.

Epuka kujenga tabia ya kulalamika kwenye jambo lolote  sababu itakujengea mfumo mbaya wa kutoweza kuona mbali na mud a mwingine huathiri mfumo mzima wa maamuzi yako kwenye kila jambo.Hakikisha unajenga uwezo bora wa kuona mbali na kufanya maamuzi ambayo unaona yatakutoa kwenye kongwa na kibao unachoona hakistali wewe kupata.

Kila unayemuona leo ni muathiriwa wa maamuzi yake ya jana  na matokeo yako ndio tunayaona leo.Ni Muhimu kujua nini unahitaji kwa wakati ujao na ndipo uanze kwa kuboresha namna unavyofanya maamuzi yako ya sasa kwa ajili ya majira yajayo ya maisha yako.

No comments: