Monday 29 June 2015

Mpinzani wa Rais Museveni kuitikisa Uganda akitokea Ulaya


Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.
 
Inadaiwa kuwa  polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.
 
Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa iliyompeleka Uingereza na Marekani huku wafuasi wake wamepanga kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.Pamoja na msafara wa magari yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.
 
Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais Museveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na hatimaye kuwania kiti cha urais.

No comments: