Tuesday, 5 September 2017

Arusha: Miili ya watoto wawili yaopolewa shimoni


Arusha. Miili ya watoto wawili ambayo haijatambuliwa imeopolewa shimoni eneo la Mji Mpya katika Mtaa wa Olkerian jijini Arusha.

Mwenyekiti wa mtaa huo, uliopo Kata ya Olasiti, Daudi Safari amethibitisha tukio hilo lililovuta wananchi wengi waliojitokeza kushuhudia kuopolewa kwa miili hiyo.

Kazi ya uopoaji ikitekelezwa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Shimo hilo lipo kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika.

Mwananchi:

No comments: