Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali haikatazi Watumishi wa Afya
kumiliki maduka ya dawa lakini ni vizuri wakazingatia kuweka maduka
hayo mbali na Vituo vya Afya vya Serikali na Hospitali ili kusiwe na
aina yoyote ya kutanguliza maslahi yao kwanza katika kutoa huduma za
dawa kwa wagonjwa.
Ameeleza
kuwa kwa sasa Serikali imejitahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na
imeamua kuanza kununua dawa kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua
kutoka kwa wafanyabiashara kama ilivyokuwa awali.
"Watendaji
badala ya kuwaandikia wagonjwa dawa zilizo kwenye orodha, wanaandika
dawa zao na kuwaambia wagonjwa wakanunue dawa kwenye maduka ya dawa.
"Hatukatazi
Watumishi kuwa na maduka ya dawa ila muhimu kuchora mstari wa dawa za
Serikali na dawa ambazo sio za Serikali.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.
No comments:
Post a Comment