Polisi
mkoani Geita wanamshikilia Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph
Kasheku (Musukuma) kutokana na vurugu zilizotokea eneo la mgodi wa GGM
Septemba 14 mwaka huu.
Mbunge
Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia
kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milion zinazotokana na
kodi ya huduma.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo jana alithibitishwa kukamatwa
kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini
Geita.
Kamanda
amesema kukamatwa kwa Musukuma ni mwendelezo wa Polisi kuwakamata
watu wote waliohusika katika vurugu zilizotokea Septemba 14.
Amesema
tayari wamekamata madiwani wengine wawili na wananchi watano na kwamba
jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi na msako wa kuwakamata wote
walioshiriki.
“Bado
tunaendelea na msako na hawa ni wahalifu kama wahalifu wengine na
sheria lazima ichukue mkondo wake na Musukuma tumemkamata sio kwamba
amekuja mwenyewe ”amesema
Kamanda
amesema kwa sasa wanaendelea na mahojiano na wakikamilisha sheria
itachukua mkondo wake na kwamba kosa la jina halina kikomo na wote
walioshiriki vurugu za kufunga barabara lazima wakamatwe na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria .
Hadi
sasa jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia madiwani kumi wa
halmashauri za wilaya ya Geita waliofunga barabara zinazoingia mgodi wa
GGM na kuharibu miundo mbinu ya maji yaliyotengenezwa na GGM kwa ajili
ya shughuli za mgodi na wananchi wa mji wa Geita katika kijiji cha
Nungwe jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Mgogoro wa madiwani na GGM
Madiwani
wa halmashauri mbili za wilaya ya Geita juzi walifunga barabara za
kuingia katika mgodi wa dhahabu wa GGM wakishinikiza kulipwa dola
12milion zinazotokana na ushuru wa huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.
Madiwani
hao wanadai fedha hizo ni haki yao kwa mujibu wa sheria kwasababu mgodi
ulipaswa kulipa ushuru wa huduma wa 0.03 toka mwaka 2004 hadi 2013 na
hawakulipa na badala yake walilipa dola 200,000 kwa kipindi chote
kinyume na sheria.
Msimamo
huo wa madiwani unapingwa na uongozi wa mgodi wanaodai kuwa mgogoro
uliopo unasababishwa na kupingana kwa sheria ambazo zote zimetungwa na
bunge.
Meneja
mawasiliano ya jamii Manase Ndoroma amesema sheria ya madini
iliwaruhusu kulipa dola 200,000 kwa mwaka huku sheria ya baraza la
madiwani ikiwa imepitisha malipo ya 0.3 jambo ambalo limesababisha
mgogoro na kwamba suluhisho pekee ni kwenda mahakamani.
Tayari
serikali mkoani hapa imewataka madiwani hao kuwa watulivu na kumsubiri
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na kamishna wa
madini kufika mkoani hapa leo Jumatatu kwa lengo la kutafuta ufumbuzi
wa mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment