Kamanda
wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na
kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi
kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya
chuma ili kuepusha madhara.
Kamanda
Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya
watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli
vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu walilookota wakati wanachunga
mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi
vibaya miguuni.
Akizungumza
kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la
bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa
taarifa ya kitu walichokiona.
Kamanda
Mkumbo amesema kuwa watoto hao wangeweza kufanya hivyo kama wangekuwa
wanakumbushwa na wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.
Kwa
upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na
ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya
msingi Nafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli
Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine
aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.
Viongozi
wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hilo ni bahati
mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juu ya
kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni
pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.
Kwa
mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo
watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote
wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutana na vitu kama hivyo na wahusika
wamekuwa wakifika mara moja na kuvichukua.
No comments:
Post a Comment