Amesema
watu hao wanadai fedha ili kuwasajili vijana na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), jambo ambalo ni kinyume na taratibu za jeshi kuajiri
vijana kwa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Mabeyo
ameonya kwamba mtu yeyote atakayetapeliwa na watu hao basi naye
atahesabika kama mmoja wa watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na
kuchukuliwa hatua mara moja.
"Maongezi
ya mtu na mtu hatuyatambui, ukitapeliwa nyamaza kimya kwa sababu
ukilalamika kwetu na wewe utachukuliwa kama sehemu ya watoa rushwa,"
amesema Jenerali Mabeyo.
Mkuu
huyo wa majeshi amebainisha njia mbalimbali ambazo wanazitumia kuajiri
vijana jeshini kuwa ni kuwachukua wale waliopitia mafunzo ya JKT au pale
wanapotaka watu wenye taaluma adimu kama vile madaktari, wahandisi au
wanasheria.
Amebainisha
kwamba jeshi linapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na
wanachukua hatua kila wanapopata taarifa ikiwa ni pamoja na kuwatafuta
wahusika na kuwakamata.
"Kuna
mmoja alikusanya vijana 15 na kila kijana akatakiwa kulipa Sh1 milioni.
Aliwapangia chumba sehemu kisha akatoweka," amesema Mabeyo na kusisitiza
kuwa wengi wanaofanya vitendo hivyo ni raia, wanajeshi ni wachache na
wanachukuliwa hatua za kinidhamu mara moja.
Kuhusu
matukio ya watu kupigwa risasi, CDF amesema wakati wote yanapotokea
matukio hayo, vyombo vya ulinzi na usalama vinakabiliana nayo mara moja
na hali inakuwa shwari.
"Kwa
ujumla hali iko shwari, huwezi kusema Tanzania siyo salama kwa sababu ya
matukio mawili ya kijambazi. Mambo tunayotaka kujiridhisha nayo kwa
sasa ni wapi wanapata silaha na wanatoka wapi," amesema Mabeyo.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment