Rais
John Magufuli ameivunja Mamlaka ya Usimamizi wa Mji Mdogo wa Kigamboni
(KDA) na sasa shughuli zake zinahamishiwa katika Manispaa ya Kigamboni.
Akizungumza
leo Jumatano,Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi amesema ametumwa na Rais Magufuli kutangaza uamuzi huo.
"Kumekuwa
na mgongano katika usimamizi wa ardhi kati ya KDA na Manispaa ya
Kigamboni, Rais ameliona hilo na kuamua kuivunja mamlaka hiyo,"amesema.
Lukuvi amesema jukumu la KDA lilikuwa kusimamia upangaji wa mji wa Kigamboni wakati hilo pia ni jukumu la manispaa hiyo.
Lukuvi
ametoa miezi sita kwa watendaji wa KDA kukamilisha makabidhiano ya
nyaraka na wao kuripoti kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.
Mapema
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amesema mgongano wa
usimamizi wa ardhi Kigamboni ulisababisha migogoro mingi ya ardhi.
Amesema pia manispaa hiyo ina upungufu wa maofisa mipango miji.
Amesema manispaa ina maofisa mipango miji watatu badala ya saba wanaohitajika.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment