Akizungumza
na Vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania, Glory Mziray amesema TFS wamekuwa wakukisanya sampuli kila
baada ya miaka miwili kutoka kwa wafugaji nyuki na kuzipeleka kwenye
Maabara za kimataifa na mara zote zimekutwa zikiwa na ubora wa hali ya
juu unaokidhi masoko yote ya kitaifa na kimataifa.
Amezitaja
tafiti mbili zilizofanyika mwaka 2016 kuwa lengo lake lilikuwa ni
kuainisha madhara ya ufugaji nyuki kwenye maeneo yanayolima Tumbaku na
ameyataja maeneo yaliyofanyiwa utafiti huo kuwa ni mkoa wa Tabora na
Kigoma
Mziray
amesema tafiti hizo zimebainisha kuwa kiwango cha nikotini
kinachopatikana kwenye asali iliyochavushwa katika mikoa inayolima
Tumbaku ni sawa na nikotini iliyopatikana kwenye asali ilivyochavushwa
na mimea mingine kama vile nyanya na miombo hivyo kiwango hicho cha
nikotini hakina madhara kwa binadamu.
Amesema
watumiaji wa asali wamekuwa wakihukumu uwepo wa nikotini kwenye
asali kwa kuangalia rangi ya asali sambamba na uchungu wa asali lakini
asali za Tanzania zinatengenezwa kwa mchanganyiko wa maua ya mimea
mbalimbali jambo ambalo linathibitishwa si nikotini peke yake ndiyo
inasababisha uchungu bali mimea mingine kama vile muarobaini.
Mziray
amewataka watumiaji wa asali kuendelea kuitumia kwa vile asali ni
chakula cha kiasili kinachotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa mimea
mbalimbali.
Ameongeza kuwa, asali ni mchanganyiko uliotokana na maji, Sukari (fruktosi, glukosi, sakrosi) madini pamoja na vitamin.
Baadhi
ya Sampuli ya asali inayopatikana katika maeneo mbalimbali za nchi.
Asali hutumika kama dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu.
No comments:
Post a Comment