Mkazi
wa Mtaa wa Mitandi Lindi Mjini, Mussa Hassan (35) amehukumiwa kifungo
cha miaka 30 jela na kulipa fidia ya Sh1 milioni, baada ya kukutwa na
makosa ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa miaka 13 aliyekuwa anasoma
darasa la sita.
Akisoma
hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Mkoa, Erasto Philly alisema Mahakama imemtia hatiani
mshtakiwa kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja katika
kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi.
Hakimu Philly alisema mshtakiwa alitenda makosa hayo Agosti 2017, kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo.
Awali,
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Emmanuel John aliiomba Mahakama kutoa
adhabu kali kutokana na mshtakiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na
umri wake ikilinganishwa na wa binti.
No comments:
Post a Comment